Swahili New Testament Bible

1st Timothy 1

1 Timothy

Return to Index

Chapter 2

1

 Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote, 

2

 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. 

3

 Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, 

4

 ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli. 

5

 Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu, 

6

 ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia. 

7

 Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo! 

8

 Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi. 

9

 Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, 

10

 bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu. 

11

 Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. 

12

 Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya. 

13

 Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa. 

14

 Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu. 

15

 Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu. 

1st Timothy 3

 

 

 

Please Click the Ads.

Clicking the Ads helps us to keep this free Bible website open for everyone.

Thanks!

 

 

 

HTMLBible Software - Public Domain Software by johnhurt.com

 


Other Items are Available At These Sites: